Jeshi la police kanda maalum ya dar es salaam linawashikilia watu 23 kwa tuhuma za kujihusisha na tuhuma za vitendo vya Udanganyifu wa mtandaoni yani Utapeli wa mtandao.
Kukamatwa kwa watu hao ni matokeo ya operation maalum iliyofanywa na kanda hiyo ya kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na Uhalifu .
Operation hiyo ilifanyika kati ya Mei 18 hadi Juni 26 ilifanyika pia katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa morogoro ambapo watuhumiwa wengine walikamatwa.
kamanda wa kanda maalum ya dar es salaam, jumanne muliro amesema waliokamatwa ni watuhumiwa waliojifanya wakuu wa shule, waganga wa kienyeji, ndugu wa waathirika, wahudumu wa makampuni ya simu au mawakala wa freemason
Amesema watuhumiwa hao huwatumia watu ujumbe mbali mbali kupitia namba tofauti za simu na kujifanya wanania ya kuwasaidia watu na baadae kuishia Kuwaibia.
miongoni walio kamatwa ni julius simon mwambura (20) ambae ni mkaazi wa ifakara sambamba na wenzake 22.
watuhumiwa haowamekutwa wakiwa na vifaa mbali mbali ambavyo wanatumia kufanyia uhalifu uoo ikiwemo kompyuta, mpakato 2, kupyuta za mezani 1, simu za aina tofauti 28, flash 2, modem za m,itandao zote na kadi za simu za mitandao mbali mbali.
katika oparesion hio wamekamatwa pia wanawake wawili kwa kosa la kufanya biashara ya ngono.

Comments
Post a Comment