ADS

Dunia Yashangazwa Poland Kupeleka Wachezaji Wake Qatar Wakisindikizwa na Ndege Ya Kivita Kucheza Kombe la Dunia

Timu zinazocheza leo kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar ni pamoja na timu ya taifa ya Poland ambayo ilivutia vyombo vya habari vya kimataifa ilipoondoka nchini mwao.

Bado kuna gumzo kuhusu jinsi ulimwengu ulivyoshangazwa na namna Timu ya Taifa ya Poland ilivyoondoka nchini mwao walipokuwa wakielekea katika jiji la Dosha nchini Qatar, kushiriki Kombe la Dunia.

Ndege iliyowabeba wachezaji wa Poland waliopaa siku ya Alhamisi ilionekana katikati ya ndege za kivita za F-16.

Mtandao rasmi wa Twitter wa timu ya Poland ulichapisha video ya jeti za F-16 zikifuata ndege ya kiraia ambayo wasomi hao walikuwamo.

"Tulipelekwa kusini mwa Poland na ndege za kivita za F-16," iliandikwa kwenye video hiyo.

Katika video hiyo hiyo, nukuu pia iliandikwa kuwashukuru marubani wa jeshi la Poland waliochukua hatua hiyo.

Picha zilizotolewa pia zilionyesha mmoja wa marubani wa F-16 akiwa na nembo ya timu ya taifa ya Poland kwenye dirisha.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya watu wawili kuuawa kwa kombora ambalo halikujulikana lilianguka nchini Poland, wakati wa vita kati ya Urusi na Ukraine.

Tangu shambulio hilo, jeshi la Poland limekuwa katika hali ya tahadhari. Vyombo vya habari vya Poland vilitangaza hatua iliyochukuliwa na jeshi kutetea timu ya taifa iliyosafiri hadi Qatar.




Comments

POP